Local Bulletins

TOHARA YA WASICHANA INGALI JUU MARSABIT KWA ASILIMIA 83 – BODI YA KITAIFA YA KUDHIBITI UKEKETAJI.

 Na Samuel Kosgei

Kuna haja ya kuendeleza hamasisho dhidi ya tabia ya kukeketea wasichana jimboni Marsabit na sehemu zote zinazofanya zoezi hilo dhalimu. Hayo ni kulingana na bodi ya kitaifa ya kupinga zoezi la ukeketaji nchini Anti FGM board.

Mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo kukabiliana na FGM nchini Bernadette Loloju amesema kuwa zoezi la ukeketaji hapa Marsabit bado inaendelezwa kwa upana na karibia jamii zote za Marsabit huku asilimia ikiwa 83.

Loloju akizungumza alipozuru kaunti ya

Marsabit kuhamasisha akina mama dhidi ya kuwakeketa wasichana wao amesema kuwa zoezi hilo linafanyika kwa asilima 15 kote nchini huku kaunti za maeneo ya wa

fugaji ikisalia kuogoza kwa zoezi hilo dhalimu kwa wasichana na wasichana.

 

“Tuko asilimia 15 kitaifa na hiyo ni punguzo kwa kuwa mwaka wa 2014 tulikuwa asilimia 21. Kaunti hatari kwa ukeketaji ni zile za maeneo ya wafugaji” akasema Bi Loloju

Amezidi kuwataka wazazi kusitisha zoezi hilo kwani inadhulumu wasichana na wanawake suala analosema kuwa ni kinyume na haki za binadamu.

Ameongeza kuwa hamasisho hilo halitakuwa kwa wanawake pekee bali pia kwa wanaume.

Anasema kuwa wote watakaoshtakiwa kwa kuendeleza ukeketaji watashtakiwa kwa kosa la unyanyasaji wa kigono na kumshika mwathiriwa sehemu zake za siri bila idhini

.Waziri wa utamaduni na jinsia katika kaunti ya Marsabit Jeremy Ledanyi kwa upande wake amesema kuwa idara yake itafufua tena kamati maalumu ya jimbo kujadili athari za ukeketaji ikiwemo kutoa hamasisho kwa wananchi wa mashinani.

Wakati uo huo amewataka viongozi wa jamii za Marsabit kuandaa vikao vya kijamii na kutangaza marufuku ya ukeketaji katika jamii zao kama hatua moja ya kukomesha au kupunguza visa hivyo.

Subscribe to eNewsletter