Local Bulletins

Waandamanaji sita wapigwa risasi katika kwenye maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha Mjini Isiolo

NA SAMAUEL KOSGEI

Maandamano ya kupinga Mswada wa Sheria ya Fedha katika Kaunti ya Isiolo yaligeuka kuwa vurugu siku ya Jumanne baada ya watu sita kupigwa risasi huku polisi wakiwahusisha waandamanaji katika mapigano.

Mmoja wa wahasiriwa alipigwa risasi mguuni huku mwingine akipigwa risasi mkononi. Wote wawili walikimbizwa katika vituo vya afya vya mjini humo kwa matibabu zaidi. Mmoja wa waliopigwa risasi ni mwanafunzi wa kidato cha nne.

Maafisa wa polisi pia waliweza kukita kambi nje ya hospitali moja katika mji wa Isiolo.

Waandamanaji walianza maandamano katika eneo la Moti Plaza na kuelekea uwanja wa Isiolo kabla ya kurejea mjini.

Baadaye walielekea katika afisi ya Mwakilishi wa Kike wa Isiolo Mumina Bonaya iliyo karibu na Kituo cha Polisi cha Isiolo.

Waandamanaji hao kisha walikusanyika mahali pa kuanzia ambapo waliimba wimbo wa taifa huku wakiimba kauli mbiu za kupinga ushuru na kuwakashifu wabunge walioupigia kura Mswada huo wiki jana.

Baadaye walielekea Barabara Kuu ya Isiolo-Moyale ambako waliwasha matairi, uamuzi ambao haukukumbatiwa na waandamanaji wote bali sehemu ya waandamanaji.

Subscribe to eNewsletter