Local Bulletins

ENEO LA MPAKANI PA KENYA-ETHIOPIA BADO LINAKUMBWA NA CHANGAMOTO ZA USALAMA

NA CAROLINE WAFORO

Huku vita vikizidi baina ya idara za usalama nchini Ethiopia na kundi la waasi la Oromo, OLF serikali ya Kenya imewahakikishia wananchi wanaoishi katika vijiji vilivyo katika eneo la Sololo mpakani pa Kenya na Ethiopia usalama wao.

Kulingana na kaimu kamishna wa jimbo la Marsabit David Saruni ni kuwa usalama umeimarishwa huku wananchi wakitakiwa kutowaficha wahalifu.

Saruni amedokeza kuwa wanaotumia ndege katika harakati za kushika doria katika eneo hilo.

Kundi la waasi la Oromo, OLF kutoka nchi ya Ethiopia huwa na hulka ya kukimbilia Kenya kufuatia makabiliano baina yao na wanajeshi wa Ethiopia na kusababisha hofu ya utovu wa usalama.

Subscribe to eNewsletter