Local Bulletins

MASHINDANO YA MICHEZO YA MUHULA WA PILI YA SHULE ZA UPILI KITENGO CHA KAUNTI NDOGO YAMEANZA NA YANAENDELEA KATIKA ENEO BUNGE LA SAKU.

NA JOHN BOSCO NATELENG

Mashindano ya michezo ya Muhula wa pili ya shule za upili kitengo cha kaunti ndogo yameanza na yanaendelea katika eneo bunge la Saku.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo katika shule ya upili ya Moi Girls, Mkurugenzi wa elimu wa kaunti ndogo ya Saku Hussein Harubu amesema kuwa mashindano haya yananuia kuwaboresha wanafunzi na kuwafanya wagundue talanta zao.

Hussein amewataka wanafunzi wote kuwa na nidhamu wakati ambapo wanacheza na wenzao kwani timu ambayo itapatkana na utovu wa nidhamu iitapugwa maruffuku kushiriki michezo hizo.

Kauli yake iliungwa mkono na mwalimu mkuu wa shule ya wasichana wa Moi Girls ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari Kenya (Kessha) tawi la Marsabit Halima Adan akisema kuwa ni sharti wadumishe nidhamu.

Wakai huo huo mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Dakabaricha Ibrahim Gere ametoa changamoto kwa wale ambao wanasimamia na kuwa marefa wa michuono hii kutopendelea shule ama timu yoyote kwani wangetaka kupata timu bora ambayo itawakilisha eneo hili katika kitengo cha kaunti mwezi ujao.

Subscribe to eNewsletter