Local Bulletins

MAONI YA JAMII KUHUSU PENDEKEZO LA KURUHUSU UPEANA VIUNGO VYA MWILI

Wakazi wa eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusu mapendekezo ya mbunge wa Laisamis Joseph Lekuton kuhusu kubuniwa kwa sheria itakayoruhusu wakenya wanaoaga dunia kupeana viungo vya mwili kwa hiari.

Baadhi ya waliozungumza na idhaa hii wameeleza kuwa hatua hiyo ni nzuri na itasaidia kuokoa maisha ya wale ambao watakuwa wanahitaji viungo hivi kwani kuna wengi ambao wamezikwa na viungo ambao si rahisi kupatikana na wakati mwingine inawafanya wengi kusafiri katika mataifa ya kigeni ili kupata viungo hivyo.

Wametaka serekali kuhakikisha kuwa kuna sheria ambao itaruhusu watu kupata viungo hivi kwa njia halali ili kuwaepusha wananchi na ufisadi ambayo itawafanya watozwe fedha nyingi sana kupata viungo hivi.

Hata hivyo wengine wametofautiana na wakisema kuwa hatua hii huenda ikahujumu haki ya binadamu kwani mtu anapokufa Anatarajiwa kupewa heshima inayofaa.

Itakumbukwa kuwa mnamo Ijumaa wiki iliyopita Mbunge wa Laisamis Joseph Lekuton alipendekeza bunge kubuni kutengeneza sheria itakayoruhusu wakenya wanaoaga dunia kupeana viungo vya mwili kwa hiari akisema hatua hiyo itasaidia wakenya wanaohitaji viungo hivyo.

Subscribe to eNewsletter