Local Bulletins

WAZIRI WA AFYA SUSAN NAKHUMICHA ASEMA BIMA MPYA YA AFYA (SHA) KUANZA KUFANYA KAZI KUANZIA MWEZI WA SABAA.

Na Samuel Kosgei

WAZIRI wa afya Susan Nakhumicha amesema kuwa bima mpya ya afya (Social Health Authority- SHA) iliyobuniwa kuchukua nafasi ya bima ya kitaifa ya afya NHIF itaanza kufanya kazi kuanzia mwezi wa saba ambao ndio mwezi wa kwanza wa mwaka wa kifedha.

Waziri Nakhumicha akizungumza alipozuru kaunti ya Marsabit kuongoza hafla ya kitaifa ya siku ya kutoa damu ulimwenguni amesema kuwa akina mama wajawazito wasiwe na wasiwasi kuwa serikali haitawapa huduma ya bure ya kujifungua kama ilivyodaiwa haopo awali badala yake waziri amesema kuwa bima mpya ya kijamii SHA itagharamia huduma za familia nzima ikiwemo watoto, mama na hata baba.

Ili kufanikisha hilo waziri amewataka wakenya wote wazima kutafuta vitambulisho ili kujiandikisha kwenye huduma ya bima mpya itakayoanzishwa kote nchini kuanzia mwezi ujao.

Aidha waziri amesema kuwa zahanati za serikali (level two)  na hospitali za ngazi ya juu kidogo (level 3) matibabu yatakua ni bure huku huduma za hospitali za juu Zaidi yakilipiwa na serikali kupitia pesa asilimia 2.75 zitakazotwa kwa wakenya walioajiriwa ili kulipia wakenya wasioweza kumudu matibabu.

Subscribe to eNewsletter