Local Bulletins

DOZI 52,000 YA CHANJO YA WATOTO YASAMBAZWA HOSPITALI ZA MARSABIT.

NA GRACE GUMATO

Afisa anayesimamia  chanjo ya Watoto kaunti ya Marsabit Abdub Boru amesema kuwa chanjo za watoto zilizoisha hapo awali sasa zimefika na zimeweza kusambazwa katika kaunti ndogo za  North Horr, Laisamis na Moyale.

Akizungumza na idhaa hii  afisini mwake Boru amesema idadi ya chanjo  ya BCG iliyofika eneo  bunge la  Moyale ni 6,000, Laisamis 5000, Saku 4000 na  North Horr ni 7,000, kwa ujumla ikiwa ni chanjo 22,000.

Chanjo ya kupitishia mdomo zilizofika eneo bunge la  Moyale ni 4,000, Laisamis 3000, Saku 6000 na North Horr 2,000, jumla ikiwa 15,000.

Aidha chanjo ya Surua (Measles) zilizofika eneobunge la  Moyale ni 4,000, Laisamis 3,000, Saku 5,000 na North Horr 3,000, kwa ujumla ikiwa ni 15,000.

Aidha Boru amesema kuwa chanjo ya HPV zinapatakana katika hospitali ya rufaa ya Marsabit akisema watoto wasichana kati ya umri wa maika 10–14 wanapaswa kupata chanjo hizo ambazo zinazuia saratani ya njia ya uzazi.

Hata hivyo Boru amewahimiza wakaazi wa Marsabit kupeleka watoto wao kupata chanjo ili kuepukana na maradhi

Subscribe to eNewsletter