Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Adano Sharamo
Bunge limepitisha kipengee tata cha mswada wa fedha kinachopendekeza ushuru wa asilimia 16 kwenye bidhaa za mafuta ya petroli kutokama asilimia 8.
Kwenye kikao jumla ya wabunge 184 wamepiga kura kuunga mkono kupitishwa kwa kipengee hicho huku 88 wakipinga.
Jumla ya wabunge 272 wa walihudhuria kikao hicho cha kupigia kura kipengee hicho muhimu.
Kipengele hicho kiliibua mjadala mkali bungeni mswada huo unapoendelea kujadiliwa kipengele kimoja baada ya kingine.
Wabunge waliochangia mswada huo hasa wa mrengo wa Azimio walikitaja kipengee hicho kuwa kitakachomuongezea mzigo mlipa kodi wakidai kwamba kuongezwa kwa ushuru huo kutaathiri sekta zote nchini.
Baadhi wa wabunge walipendekeza kipengele hicho kuondolewa kabisa huku wengine wakipendekeza kiwango hicho kusalia kuwa kile cha awali cha asilimia 8.
Ikumbukwe kipengele hicho cha ailimia 16 kimekuwapo kabla ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta kupunguza kiwango hicho hadi asilimia 8.