Local Bulletins

Wakaazi wa Marsabit Watolewa Wito wa Kujitokeza Kufanyiwa Vipimo vya Macho

PICHA: KWA HISANI

Na Samuel Kosgei

Wakaazi wa Marsabit wametolewa wito wa kujitokeza kufanyiwa uchunguzi na vipimo vya macho mara kwa mara kabla ya kupoteza uwezo wa kuona.

Mhudumu wa afya kitengo cha macho katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Galgalo Arero akizungumza nasi alisema kuwa kwa muda wengi wa wakaazi wa Marsabit wanatembelea hospitalini baada ya kupoteza uwezo wa kuona suala analosema halifai katu.

Idara ya afya ya kaunti ya Marsabit na wafadhili wake kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa wiki hii watakuwa na kambi ya kushughulikia matatizo ya macho mjini Laisamis ambapo kufikia sasa watu zaidi ya 200 wamefanyiwa vipimo huku wengine Zaidi ya 100 wakifanyiwa upasuaji wa macho ili kurekebisha kero la kutoona.

Idadi kubwa ya watu ambao anasema waliotembelea kambi hiyo ya Laisamis kusaka matibabu ya macho ni wazee wa umri wa makamo ambao alitaja ndio wameathirika sana. Wanalenga kuhudumia watu Zaidi ya 300.

Subscribe to eNewsletter