Local Bulletins

Uchunguzi waanzishwa kuhuisiana na kifo cha balozi wa Amani kaunti ya Isiolo Bi.Elizabeth Ibrahim.

Balozi wa Amani kaunti ya Isiolo Bi.Elizabeth Ibrahim
Picha;Hisani

Na Silvio Nangori,

Polisi katika kaunti ya Isiolo wameanzisha uchunguzi kufuatia kisa ambapo balozi wa amani bi.Elizabeth Ibrahim ameuawa eneo la Kambi Garba kaunti ya Isiolo.

Imeripotiwa kwamba Elizabeth Ibrahim alivamiwa na jirani yake ambaye alimdunga kwa kisu mara kadhaa na kufariki papo hapo.

Wakaazi wa eneo hilo walikuwa wamejawa na ghaghabu walivamia mshukiwa wa mauaji na kumchapa kabla ya kuokolewa na polisi.

Kwa Sasa mshukiwa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Isiolo Kabla ya kufikishwa mahakamani.

Kuligana na taarifa ambazo hazijadhibitishwa ni kwamba mwanamke huyo aliuliwa kutokana na mzozo wa ardhi eneo hilo,kisa ambacho kimekashifiwa vikali na viongozi na wakaazi  wa Isiolo kupitia mitandao ya kijamii.

Huku hayo yakijiri

Kwa mara nyingine wito umetolewa kwa wakaazi kaunti ya Isiolo kuwachagua viongozi ambao wanasera za kuwasaidia wananchi badala ya kumchagua kiongozi kwa msingi ya chama chake.

Wito huu umetolewa kwa John Kibaso mkaazi wa wadi ya Bulapesa ambaye amesema siasa za uchaguzi ujao zinafaa kuwa kwa misingi ya sera za wagombea ili kuleta mabadiliko katika jimbo la isiolo.

Wakati uo huo Kibaso ambaye pia ametangaza kuwania kiti cha wadi ya Bulapesa amewataka wakaazi Isiolo kutowachagua viongozi ambao wamekuwa na mazoea ya kuchaguliwa na kuwatelekeza wapiga kura.

Subscribe to eNewsletter