Local Bulletins

Kaunti ya Garissa inatarajia kuwapa chanjo watoto 165,000 walio kati ya miezi 9.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Wizara ya afya katika kaunti ya Garissa inatarajia kuwapa chanjo watoto 165,000 walio kati ya miezi tisa dhidi ya ugonjwa wa ukambi na Rubella.

Kwenye mkutanao uliowaleta pamoja washikadau kwenye sekta ya Afya katika kaunti hiyo mkurugenzi wa Afya ya magonjwa ya kusambaa kaunti ya Garissa Ibrahim Gedi amesema kuwa shughuli hiyo itangoa nanga hapo kesho huku ikitarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa.

Gedi vilevile amesema kuwa watoto wanaolengwa watachanjwa pahala popote watakapopatikana.

Ametaja kuwa kaunti hiyo inapitia changamoto nyingi kwa kuwa inapakana na nchi jirani ya Somalia ambayo watoto wengi hawapati chanjo hiyo huku akiwataka wazazi kutopuuza zoezi hilo.

Subscribe to eNewsletter