Local Bulletins

Rais Uhuru Kenyatta yuko nchini Djibouti, kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Ismail Omar Guelleh.

Rais Kenyatta Alipotua Nchini Djibouti.
Picha; Ikulu

Na Adano Sharawe.

Rais Kenyatta,ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliwasili nchini humo Jumamosi asubuhi akiwa ameandamana na waziri wa mashauri ya kigeni Raychelle Omamo.

Viongozi wengine wanaohudhuria sherehe hiyo ni waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, rais Muse Bihi Abdi wa Somaliland na waziri mkuu wa Somalia Mohamed Roble.

Rais Ismail Omar Guelleh alichaguliwa kwa muhula wa tano, kwa kupata zaidi ya asilimia 98 ya kura zilizopigwa,na kumshinda mpinzani wake wa pekee, mfanyabiashara Zakaria Ismail Farah.

Takriban wapiga kura 215,000 walishiriki uchaguzi huo katika taifa hilo lililo na watu milioni moja.

Kenya na Djibouti zina uhusiano mwema wa kidiplomasia.

Rais Guelleh alizuru Jiji la Nairobi tarehe 9 mwezi May kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili ambapo alifanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta.

 

Subscribe to eNewsletter