Local Bulletins

Kenya Yaungana Na Ulimwengu Kusherehekea Siku Ya Wanyamapori Duniani

Picha;Hisani

By Silivio Nangori,

Hii leo ikiwa ni siku ya wanyama pori Duniani taifa linaadhimisha siku hiyo katika eneo la Shimoni kaunti ya Kwale.

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la kuwalinda wanyama pori Kaskazini mashariki mwa nchi Robert Obrein ametaja siku hii kuwa muhimu sana katika kuhamasisha wananchi kuhusiana na utunzaji wa misitu na wanyama pori.

Obrein amesema kwamba ni jukumu la kila mmoja kuwalinda kutokana na muhimu wake katika uchumi wa nchi.

Kwa mara ya kwanza nchi ya Kenya haijapoteza kifaru yeyote tofauti na mwaka wa 2013 ambapo vifaru 59 waliuawa. Ameongeza kusema siku hii Ya leo lengo kuu ni kupunguza Zaidi uwindaji haramu wa vifaru.

Subscribe to eNewsletter