Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Jillo Dida Jillo,
Wanaume 12 wamefikishwa,mbele ya mahakama ya Marsabit kwa kosa ya kuendesha piki piki bila stakabadhi hitajika.
12 hao walikamatwa na maafisa wa trafiki jumapili tarehe 31 mwezi Januari mwaka huu katika soko la Merile kaunti ndogo ya Marsabit Kusini.
Wameshtakiwa kwa makosa ya kuendesha piki piki kwenye barabara ya umma bila kuwa na Leseni kinyume na sheria ya Kenya kifungu cha 103 B(5) na kifungu cha 103 B(7).
Wanakabiliwa na makosa ya kukosa Leseni, Bima, ukiukaji wa sheria za trafiki.
Kumi na wawili hao ni pamoja na David Lepatti, Adan Ali, Peter Esimonte, David Lemassio, Leopelie Ltarra, Segelan Galchui, Joseph Ortoyo, Nkarus Orgoba, Juma Dafardai, Samuel Lenerima, Edward Ejore na Joseph Kamurte.
Katika uamuzi wake hakimu mkaazi wa marsabit Collins Ombija amemhukumu mshatakiwa Joseph Kamurte kifungu cha mwezi moja gerezani ama faini ya shilingi Elfu Nne kwa kila kosa linalomkabili.
Washtakiwa David Lepatti, Adan Ali na Peter Esimotte wote wamehukumiwa kifugu cha mwezi 1 gerezani ama faini ya shilingi elfu 5 kila mmoja huku washtakiwa Leopelie Ltarra na Segelan Galchui wakipigwa faini ya shilingi Elfu Tisa ama kifungu cha Miezi 2 gerezani.
Joseph Ortoyo amehukumiwa kifungo cha mwezi moja au faini ya shilingi Elfu mbili, mshtakiwa Nkarus Orgoba amehukumiwa kifungo cha Miezi 3 au faini ya shilingi elfu 9, Juma Dafardai faini ya shilingi elfu 16 ama kifungo cha meizi 3 na Edward Ejore faini ya shilingi 2500 au kifungo cha mwezi moja gerezani.
Aidha washtakiwa David Lemassio na Samuel Lenarima wamewekwa chini ya uangalizi wa mwiezi 6 na wiki mbili mtawalia.
Show quoted text