Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Picha; Hisani
By Mark Dida.
Kamishna Wa Kaunti Ya Marsabit Paul Rotich Amesema Zaidi Ya Asilimia 54 Ya Wanafunzi Katika Shule Mbalimbali Katika Kaunti Ya Marsabit Wamerudi Shuleni.
Rotich Ameelezea Kuridhishwa Na Utayari Wa Shughuli Hiyo Kwenye Shule Za Kaunti Hii Na Aslimia Ya Watoto Waliorejea Shuleni Tangu Siku Ya Jumatatu Licha Ya Changamoto Ya Mawasilino Kwa Wasimamizi Wa Shule Za Mashinani Ambao Wamenakili Idadi Ndogo Ya Wanafunzi Waliorejea Shuleni.
Rotich Amesema Ni Sharti Kila Mtoto Arudi Shuleni Wakiwemo Wale Waliyopachikwa Mimba Na Waliojifungua.
Amewaonya Wazazi Ambao Hawajawapeleka Watoto Wao Shuleni Kwamba Watachukuliwa Hatua Kali Na Serikali.
Aidha, Rotich Ametoa Wito Kwa Washikadau Wakiwemo Wazazi, Viongozi Wa Kidini Na Kisiasa Kushirikiana Na Maafisa Wa Elimu Kuhakikisha Wanafunzi Wanarejea Shuleni.
Rotich Amewataka Walimu Kuhakikisha Wanafunzi Wanaosha Mikono,Kuvaa Barakoa Na Kutotangamana Kwa Karibu Na Wenzao Ili Kuzuia Msambao Wa Ugonjwa Wa Corona.
Wakati Uo Huo, Rotich Amewatahadharisha Wakazi Wa Kaunti Hii Dhidi Ya Kukiuka Masharti Yaliyowekwa Kukabiliana Na Janga La Corona Kwa Kuzingatia Masharti Yote Ya Afya Kama Vile Kutotangamana Kwa Karibu, Kuvaa Barakoa, Kunawa Mikono Na Kuepuka Kuzurura Zurura.