Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Adano Sharawe
Halmashauri ya kuthibiti sekta ya kawi na mafuta (EPRA) imefunga kituo cha Gumi kilicho eneo la Sololo kaunti ya Marsabit kwa kuuza mafuta yaliyochanganywa.
Kituo cha Gumi ni kati ya vituo 16 vya mafuta ambavyo Epra imefunga kuuza humu nchini.
Kwenye taarifa, halmashauri hiyo ilisema ilifanya ukaguzi kati ya mwezi oktoba na desemba , ambapo jumla ya sampuli 5,574 za mafuta zilipimwa katika vituo 1,151 vya petroli.
Kutoka kwa vipimo vya sampuli hizo, asilimia 98.61 ya vituo hivyo vilipatikana kuuza mafuta safi huku vituo 16 vikipatikana kuuza mafuta yaliyochanganywa.
Jijini Nairobi, kituo cha petrol cha Riva kilichoko barabara ya Murang’a kimefungwa kwa kuuza petrol ya Super iliyochanganywa na mafuta taa.
Vituo vitatu huko Homa Bay vimefungwa na halmashauri hiyo ambapo viwili vilipatikana vikiuza mafuta yaliyokusudiwa kuuzwa nje ilhali cha tatu kilipatikana kikiuza diesel iliyochanganywa na mafuta taa.
Kituo cha mafuta cha Triple M na National Oil Kianjai, vyote vya Meru vilipatikana kuwa vinauza mafuta yaliyochanganywa.
Kituo cha mafuta cha Safe Line mjini Nakuru pia kimefungwa kwa kuuza diesel ya kuuzwa nje.