Wadau wasisitiza usawa katika malezi na maendeleo ya watoto.
Na Sabalua Moses
Afisa mkuu wa programu kutoka shirika la Compassion, Ronaldo Fandia, amesema watoto wote wanapaswa kupata fursa sawa bila ubaguzi wa kijinsia.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika Kaunti ya Marsabit, Fandia amesema mara nyingi haki za mtoto wa kike hupewa uzito mkubwa, huku mtoto wa kiume akisahaulika, hasa katika jamii za wafugaji.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa maafisa wa afya nyanjani almaarufu kama CHPS katika eneo la Jirime, Amina Galgalo, amesema watoto wengi wa maeneo ya mashinani wanakumbwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo dhuluma za kijinsia na ukosefu wa huduma muhimu za kijamii.
Naye muuguzi katika Hospitali ya Jirime, Rahma Abdi, amesema watoto wengi wanahitaji msaada wa kiafya kutokana na tatizo la utapiamlo. Ameitaka serikali pamoja na wadau wengine kuongeza juhudi za kuwasaidia watoto walio katika mazingira hatarishi ili kuboresha afya na ustawi wao.



Post Comment