Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Isaac Waihenya.
Klabu ya Gor Mahia imemtambulisha kocha wao mpya Jonathan McKinstry kuchukua nafasi ya Mjerumani Andres Spiers ambaye aliigura klabu klabu hiyo mwezi uliopita.
McKinstry raia wa Ireland ametambulishwa hii leo kwa umaa na mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier huku akisaini mkataba wa miaka miwili.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 37 amewahi kuzinoa timu za taifa za Uganda, na Rwanda na pia vilabu mbalimbali katika mataifa ya Bangladesh,Luthuania na Siera Leone.
McKinstry aliongoza timu za taifa ya Uganda kati ya mwaka wa 2019 na 2021 na pia timu ya taifa ya Rwanda mnamo 2015.
Akizungumza wakti wa hafla hiyo McKinstry amesema kuwa mojawapo ya malengo yake ni kuisaidia klabu hiyo kunyakua taji la ligi kuu hapa nchini na kurejesha ubabe wake wa zamani hapa nchini n ahata barani Afrika.
Mwalimu huyo anajiunga na Gor Mahia siku chache baada ya miamba hao wa soka nchini kutia saini mkataba wa miaka mitatu wa shilingi milioni 229.5 na kampuni ya bahati nasibu BetAfriqe.