Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Orodha ya wagombea katika nafasi mbalimbali za FKF Marsabit yatolewa.
Huku uchaguzi wa kuwania nafasi mbalimbali katika shirikisho la soka nchini Kenya FKF ukitarajiwa kufanyika hivi karibuni wagombea kutoka maeneo mbalimbali wamejitokeza kuwania nafasi za uongozi katika kaunti ya Marsabit.
Miongoni mwa nafasi zinazogombaniwa ni pamoja na Uenyekiti,katibu, mweka hazina,mwakilishi wa akina mama na mwakilishi wa vijana.
Katika nafasi ya mwenyekiti, mwenyekiti wa sasa Mohamed Nane Shege anasaka kuhifadhi nafasi yake wakati huu akimteua Getito Ndiritu Gethu ambaye ni katibu wa sasa kuwa naibu wake.
Nane anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Godana Roba Adi ambaye amemteua Samson Sausen Nicholas kuwa naibu wake.
Katika nafasi ya katibu,Ali Awadh Abdalla ambaye ni naibu mwenye kiti wa sasa na Imran Said Harub,watapambania wadhifa huo.
Aidha Abdulkarim Abdulrahman pamoja na Adan Mohamed Dulacha wanapambania nafasi ya mwekahazina katika uchuguzi huo unaotarajiwa kuandaliwa tarehe 7 mwezi disemba mwaka huu.
Mwakilishi wa akina mama wa sasa Jatttane Jeremiah Haile atapambana na Dorcas Nasujaa Choya katika nafasi hiyo huku, Adano Ramata Galgalo na Abdikadir Wario Dadacha wakimenyana katika nafasi ya mwakilishi wa vijana.
Viongozi wa FKF wamesisitiza umuhimu wa uchaguzi huo kufanyika kwa njia ya haki, uwazi, na amani ili kuhakikisha matokeo yanakubalika na washikadau wote.