Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Waihenya Isaac,
Klabu ya Ulinzi Stars imetoka sare ya magoli mawili na klabu ya Western Stima Katika mechi iliyosakatwa hii leo Katika uwanja wa michezo wa Afuraha mjini Nakuru.
Wanajeshi Ulinzi stars walikuwa wa kwanza kucheka na wavu kupitia mchezaji mkongwe Oscar Musa Wamalwa kunako dakika ya 14 katika kipindi cha kwanza, kabla ya mchezaji Barrona Oketch kuisawazishia klabu ya Western Stima kunako dakika ya 47 katika kipindi cha pili.
Kunako dakika ya 75 Kiungo Elvis Nandwa aliwapa wanajeshi uongozi kwa mara nyingine kabla ya Martin Mbaruku kufuta uongozi huo na kulazimisha vilabu hivyo kugawana alama.
Sare hiiyo imeiacha Klabu ya Ulinzi stars Katika nafasi ya 8 kwa alama 14 baada ya mechi 11 huku Western wakisalia Katika maeneo hatari ya kushushwa daraja – nafasi ya 17 kwa alama 7 bada ya kushiriki mechi 11.
Katika mechi nyingine iliyopigwa hii leo, Klabu ya Mathare United imeinyuka Nzoia Sugar kwa goli moja kwa nunge ugani Kasarani.
Bao la Kipekee la vijana wa mtaani Mathare United lilipachikwa wavuni kunako dakika ya 57 kupitia mchezaji James Kinyanjui.
Mathare sasa wanashikilia nafasi ya 16 kwa alama 8 baada ya mechi 8 huku nzuia Sugar wakiw akatika nafasi ya 12 kwa alama 11 baada ya mechi 11.