Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Waihenya Isaac,
Shirikisho la Raga Duniani limetangaza ratiba ya mechi za Kombe la Bara Afrika zitakazotumiwa kama mashindano ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2023.
Timu ya taifa ya Kenya ya raga ya wachezaji 15 kila upande maarufu kama Simbas itaanza kampeni yake dhidi ya Senegal Julai 3 jijini Nairobi, kisha vijana hao wanaonolewa na kocha Paul Odera watakabiliana na Zambia ugenini.
Odera alitaja majina ya wachezaji 102 watakaoanza, na kusema wachezaji hao watapunguzwa hadi 50 kabla ya orodha ya mwisho ya wachezaji 30 kutangazwa, ambao wataiwakilisha Kenya kwenye Kombe la Afrika.
Kocha Odera atarajiwa kuwa makini na mechi hizi kwani Kenya haijawahi kuingia Kombe la Dunia la raga ya wachezaji 15 huku akipania kuandikisha historia hiyo.