Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Kocha Arsene Wenger Akiwa Ugani Emirates.
Picha Hisani
By Waihenya Isaac.
Afisa Mkuu Mtendaji Wa Klabu Ya Arsenali Vinai Venkatesham Ameripotiwa Kuwasiliana Na Arsene Wenger Juu Ya Uwezekano Wa Kurudi Uwanjani Emirates.
Wenger Aliiongoza Arsenal Kutwaa Mataji Matatu Ya Ligi Kuu Na Vile Vile Kombe La FA Kabla Ya Kuondoka Baada Ya Miaka 22.
Meneja Huyo Mashuhuri Alijiuzulu Kutoka Wadhifa Wake Mnamo Mwaka 2018 Baada Ya Miaka Yake Ya Mwisho Klabuni Kukumbwa Na Maandamano Na Hasira Kutoka Kwa Mashabiki Wa Klabu Hiyo.
Baada Ya Kuondoka Ugani Emirates, Inasemekana Kuwa Kocha Arsene Wenger Aliapa Kutokanyaga Tena Uwanja Wa Emirates Ila Inaarifiwa Kuwa Afisa Mkuu Mtendaji Vinai Venkatesham Anafanya Njama Ya Kumrudisha.
Kwa Sasa Washika Bunduki Wamo Katika Nafasi Ya 15 Kwenye Jedwali La Ligi Kuu Nchini Uingereza Chini Ya Ukufunzi Wa Mikel Arteta Na Alama 13 Kutoka Kwa Mechi 11.
Arteta Anakabiliwa Na Shinikizo Baada Ya Kupoteza Mechi 4, Kushida 1 Na Kutoka Sare 1 Katika Mechi 6 Za Mwisho Za Arsenali Katika Ligi Ya Primia.