Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…
January 15, 2025
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na mapendekezo ya Senata wa kaunti ya Kiambu Karungo Thungwa ya kutaka muhula wa kutawala kupunguzwa kutoka miaka mitano hadi miaka minne. Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya radio jangwani, wamesema kuwa wanaunga mkono mswaada huo wa kupunguza muda wa kuhudumu kwa viongozi[Read More…]
Mifugo katika lokesheni za Balesa, Dukana na El Adhe Eneobunge la North Horr huenda ikakumbwa na ukosefu wa lishe baada ya moto unaosambaa kwa kasi kuteketeza sehemu kubwa ya malisho. Chifu wa Dukana Tuye Katello ameambia shajara kuwa moto mkubwa ulioanzishwa na mfugaji mmoja umeenea kwa kasi kutokana na wingi[Read More…]
Watu 300 wanatarajiwa kupewa mafunzo na kujiunga na kikosi cha maafisa wa akiba NPR jimboni Marsabit. Hii ni baada yao kupigwa msasa katika zoezi lilifanyika kuanzia wiki jana na kuongozwa na OCPD wa maeneo mbalimbali kwa ushirikiano na machifu. Serikali itatoa mwelekeo ambapo 300 hawa watapewa mafunzo na kisha kutumwa[Read More…]
FAIDA inayopatikana kwa kuuza bidhaa za Moyale Kenya kwenda Ethiopia imetajwa kupungua kutokana na kushuka kwa thamani na kudidimia kwa sarafu ya Ethiopia Birr. Naibu Mwenyekiti wa chama cha wanabiashara KNCCI tawi la Marsabit Alinur Mumin ameambia shajara kuwa kushuka kwa nguvu ya sarafu hiyo imeteremsha faida na mchakato mzima wa[Read More…]
Ni watu wachache sana walioelewa jinsi ya kutumia fedha zao ipasavyo. Haya ni kwa mjibu wa mataalam wa maswala ya kifedha John Maina. Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Maina amesema kuwa watu wengi wanapata pesa ila wanaojua namna ya kuzitumia vyema ni wachache mno huku[Read More…]
Afisa anayesimamia usafi wa chakula katika kaunti ndogo ya Saku Goba Boru amewaonya wale wale wanaozugusha vyakula mitaani katika kaunti ya Marsabit kuwa wakabiliwa kisheria. Akizungumza na Radio Jangwani, Boru amesema kuwa zoezi la uchuuzi wa chakula ni kinyume cha sheria kwani vingi vya vyakula hivyo vinavyozungushwa mtaani havijafikia vigezo[Read More…]
Serekali ya kaunti imeweka mikakati kuhakikisha kwamba watoto wa kurandaranda wanashugulikiwa vilivyo na kurejeshwa shuleni. Hayo yamekaririwa na afisa mkuu katika idara ya jinsia kaunti ya Marsabit Anna Maria Ndege. Akizungumza wakati wa mkao wa kuzindua kamati itakayoshughulikia maswala ya watoto wanaorandaranda katika kaunti ya Marsabit chini ya usimamizi wa[Read More…]
Hali ngumu ya uchumi imechangia changamoto wanayopitia wanawake katika kaunti ya Marsabit ambayo inasababisha mavurugano katika familia. Haya ni kwa mujibu wa mtetezi wa haki za kibinadamu kutoka shirika la MWADO, Dale Ibrahim. Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, Dale amesema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa imechangia pakubwa[Read More…]
Tutawakamata wazee ambao wataendeleza ndoa za mapema katika eneo la Loiyangalani. Haya ni kwa mujibu wa naibu kamishna wa eneo la Loiyangalani Stanley Kimanga. Kimanga amesema kuwa ni jukumu la wazee kulinda haki ya mtoto msichana na kuwaepusha na mila potovu ambayo imepitwa na wakati. Akizungumza na idhaa hii kwa[Read More…]
Takriban vijana 1,500 jimboni Marsabit wanatarajiwa kunufaika na kazi mazingira mpango wa kushughulikia hali ya anga na ambao ulizinduliwa na rais William Ruto mwezi septemba. Mpango huu ni mojawepo ya mbinu ya kuunda nafasi za kazi kwa mamilioni ya vijana ambao hawajaajiriwa nchini na ambao ulichukua nafasi ya Kazi Mtaani[Read More…]