Highlights

Lekuton ataka doria za polisi kuimarishwa eneo la Yel, Kargi baada ya mkazi kupigwa risasi maajuzi mpakani.

Na Samuel Kosgei

Mbunge wa Laisamis, Joseph Lekuton, amemtaka Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen kuamrisha kuimarishwa kwa doria za polisi katika eneo la Yel, Kargi, kaunti ya Marsabit, kufuatia tukio la mtu mmoja kupigwa risasi juzi kutokana na mzozo wa malisho wakati huu wa kiangazi.

Akizungumza bungeni Jumatano, Lekuton alisema kuna haja ya dharura kwa idara ya usalama kuimarisha ulinzi katika eneo hilo la mpaka wa jamii mbili, ili kuzuia visa vya mara kwa mara vya migogoro.

Amesema migongano imeongezeka hasa kipindi hiki cha ukame, huku wafugaji wakizozania maeneo ya malisho na maji.

Akijibu hoja hiyo bungeni, Waziri Murkomen alilihakikishia bunge kuwa wizara yake, kwa ushirikiano na Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, itachukua hatua za haraka kushughulikia mzozo huo wa mpaka kati ya eneobunge la Laisamis na North Horr.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

1 comment

comments user
Santiago

Every time I tune in, I feel connected to home. Massive respect to Radio Jangwani for uplifting our community!

Post Comment