Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Matayarisho Ya Kumpumzisha Aliyekuwa Askofu Wa Jimbo Katoliki La Marsabit Askofu Ambrose Ravasi Yanaendelea.
Kwa Mujibu Wa Vika Jenerali Wa Jimbo Katoliki La Marsabit Ambaye Pia Na Mkugenzi Mkuu Wa Radio Jangwani Padre Ibrahim Racho Ni Kuwa Ibada Ya Kwanza Ya Wafu Itandaliwa Jumatano Tarehe 4 Mwezi Huu Wa Novemba Katika Kanisa La Mtakatifu Maria Consolata Eneo La Westlands Jijini Nairobi Kabla Ya Mwili Wake Kusafirishwa Hadi Hapa Mjini Marsabit Alhamisi 5 Mwezi Huu.
Mwili Wake Ravasi, Utapokelewa Katika Uwanja Mdogo Wa Ndege Hapa Marsabit Na Viongozi Wa Kanisa Wakiongozwa Na Baba Askofu Peter Kihara Na Kusafirishwa Hadi Kanisa Kuu La Katoliki Mjini Marsabit Ambapo Ibada Ya Wafu Ifanyika Saa Nane Mchana Ikiongozwa Nae Baba Askofu Peter Kihara.
Siku Io Hiyo Alhamisi Misa Ya Kesha Itakayoongozwa Na Baba Askofu Peter Kihara Itandaliwa Pia Katika Kanisa Lilo Hilo Hapa Marsabit.
Wananchi Wa Jimbo La Marsabit Watakuwa Na Fursa Ya Kuutazama Mwili Wa Askofu Ambrose Ravasi, Mchana Na Hata Usiku Alhamisi Hiyo.
Ijumaa 6 Mwezi Huu Ibada Nyingine Ya Wafu Itandaliwa Katika Kanisa Hilo La Maria Mtakatifu Consolata Kuanzia Saa Kumi Na Mbili Unusu Hadi Saa Moja Unusu.
Ibada Hiyo Itaongozwa Na Baba Askofu Wa Jimbo Katoliki La Mararal Askofu Virgilio Pante.
Baadae Kuanzia Saa Nne Asubuhi Ibada Ya Wafu Itandaliwa Papo Hapo Na Kisha Mwili Wake Kusafirishwa Hadi Katika Eleo La Maombi La Maria Mfariji Shrine Kwa Mazishi.
Radio Jangwani Inawapa Pole Wamisionari Wa Konsolata Hapa Nchini Na Waumini Wa Jimbo Katoliki La Marsabit.
Raha Ya Milele Umpe Ee Bwana, Na Mwanga Wa Milele Umwangazie; Apumzike Kwa Amani.
Amina.