Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Samuel Kosgei
Idara ya polisi mjini Marsabit imesema kuwa imeweka mikakati mwafaka ya kukomesha uhalifu na wizi ambao umeonekana kuongezeka mjini Marsabit siku za hivi karibuni.
Afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Marsabit Edward Mabonga ameambia shajara kuwa tayari polisi wana habari kuhusu malalamishi hayo ya umma na hivyo tayari polisi wataimarisha doria usiku na mchana ili kukomesha hulka hiyo ya wiizi na uhalifu.
Kauli yake OCS Mabonga inajiri siku chache baada ya wezi wenye silaha kujaribu kuibia duka moja eneo la Shauri Yako viungani mwa mji wa Marsabit wikendi iliyopita.
Maeneo ambayo yametajwa kuongezeka kwa visa vya uhalifu na wizi viungani mwa mji wa Marsabit, ni pamoja Karantina, Kiwanja Ndege, Majengo na Shauri Yako.