County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

ZAIDI YA WATU 20 WAADHIRIKA NA UGONJWA WA UPELE MAARUFU SCABIES KATIKA KIJIJI CHA BURURI,MOYALE KAUNTI YA MARSABIT.

Na Isaac Waihenya,

Wakaazi katika kijiji cha Bururi eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit wameitaka idara ya afya hapa jimboni kutuma msaada wa kimatibabu katika eneo hilo ili kushughulikia ugonjwa unaokisiwa kuwa ni Upele maarufu Scabies.

Wakizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu wakaazi hao wametaja kwamba tayari watu zaidi ya 20 ikiwemo watoto wadogo wameadhirika na ugonjwa huo na ambao wanataja kuwa  ulizuka miezi mitatu iliyopita.

Wametaja kwamba hawajapata matibabu kutokana na kukosekana kwa dawa katika kituo cha afya cha eneo hilo huku wakilazimika kusafiri hadi mjini Moyale kusaka matibabu.

Aidha wamekariri kuwa wanafunzi na ambao wameadhirika pia na ugonjwa huo wamekosa kuhudhuria masomo shuleni.

Subscribe to eNewsletter