Rais Ruto asikitikia hali ya usalama nchini DRC haswa ukanda wa unaokaliwa na waasi wa M23.
January 27, 2025
NA NAIMA
Wizara ya afya katika kaunti ya Marsabit imetihibitisha kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa wa Surua au MEASLES jimboni.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani afisini mwake waziri wa afya jimboni Marsabit Malicha Boru amedokeza kuwa ugonjwa huu umeripotiwa katika maeneo bunge ya Moyale na Northhorr.
Visa vitatu vimeripotiwa Moyale huku eneobunge la North Horr likiripoti visa vinne kama anavyoeleza.
Malicha ameainisha kuwa visa vya ugonjwa huu vikizidi vitatu basi inaorodheshwa kuwa mkurupuko huku akidokeza mikakati wanayoweka kukabiliana na ugonwja wa measles.
Na kuhusiana na ugonjwa Mpox waziri amedokeza kuwa wizara ya afya ipo ange pamoja na kuhamasisha wakaazi kuhusiana na kuenea kwake.
Dalili za ugonjwa mpox ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo na misuli kuuma.
Mara baada ya homa, upele unaweza kutokea, mara nyingi huanza kwenye uso kisha kuenea kwenye sehemu nyingine za mwili, mara nyingi viganja vya mikono na nyayo za miguu.
Ugonjwa huu wa mpox umetwajwa kusababishwa na wanyama. Wakaazi jimboni marsabit na wakenya kwa ujumla wakionywa dhidi ya kula nyama ya wanyama wanaowindwa ili kuziua kuenea kwa virusi hivi vya mpox nchini.
Visa vya mpox tayari vimeripotiwa katika kaunti za taita taveta na Busia