Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na JB Nateleng & Naima Abdullahi,
Wanabodaboda katika kaunti ya Marsabit wametoa Rai kwa idara ya usalama jimboni kuweza kuangazia upya maamuzi ya kupiga marufuku uendeshaji wa boda boda masaa ya usiku.
Baadhi ya waliozungumza na idhaa hii wamesema kuwa itakuwa ni afueni iwapo idara ya usalama itaandaa mkao na wanabodaboda jimboni na kuweka mikakati ambayo itawasaidia wanabodaboda wanaofanya kazi usiku kwani wengi wao wanategemea biashara hiyo kulisha familia zao.
Wamesisitiza kuwa iwapo serekali itashirikiana na wanaboda boda wote jimboni basi watakuwa wakipata ripoti ya uahalifu hivyo kukomesha na kutokomeza uvunjaji wa maduka nyakati za usiku.
Aidha wameitaka serekali kuwapiga msasa wanabodaboda wote katika eneo la bunge Saku ili kuweza kubaini wanahlifu wanaojificha na kujitokeza wakati wa usiku kutekeleza wizi wa uvunjaji wa maduka.
Hata hivo Mmoja wao ameunga mkono hatua hiyo akisema kuwa itasaidia katika kuboresha usalama wa wanabodaboda na pia kupunguza visa vya maduka kuvunjwa wakati wa usiku.