Gavana wa Marsabit Mohamud Ali apongeza rais Ruto kwa kuondoa hitaji la kupigwa msasa wakati wa kusaka kitambulisho….
February 6, 2025
NA CAROLINE WAFORO
Idara ya misitu katika kaunti ya Marsabit sasa inasema kuwa imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa moto unaoshuhudiwa katika kaunti jirani ya Isiolo hauenei hadi katika jimbo hili la Marsabit.
Akizungumza na shajara ya radio jangwani afisini mwake mhifadhi wa msitu wa Marsabit Mark Lenguro amesema kuwa idara yake imetuma wataalam katika maeneo ya shurr pamoja na maeneo mengine yanayopakana na kaunti ya isiolo ili kuhakikisha kuwa moto huo hauenei.
Lenguro pia amewatahadhari wananchi dhidi ya kuwasha moto kiholela.
Moto huo jimboni Isiolo umteketeza ardhi kubwa ya malishi huku wakaazi wakilaumu seriklai kuu na ile ya kaunti kwa kuwatelekeza