Wazazi eneo la Laisamis,kaunti ya Marsabit waonywa dhidi ya kutowapeleka wanao shuleni.
January 6, 2025
Wakaazi wa Marsabit wametahadharishwa kuhusu hatari za mchezo wa kamari, ambao umeanza kuathiri maisha ya vijana na hata uhusiano wa ndoa katika jamii. Akizungumza na idhaa hii, Sheikh Mohamed Nur, kiongozi wa kidini katika msikiti wa Jamia kaunti ya Marsabit, amesisitiza kwamba kamari ni haramu katika dini na kwamba ni muhimu kwa watu kujiepusha nayo.
Sheikh Mohamed ameelezea jinsi kamari, hasa ile inayochezwa kwa njia ya simu, imeleta madhara makubwa kwa jamii.
Ameonya kuwa kamari inachangia katika kuongezeka kwa ufukara, talaka, na hata wizi, kwani wachezaji wanajikuta wakihitaji fedha ili kufanikisha tabia hii hatari.
Aidha, Sheikh Mohamed amewakumbusha wakaazi kuhusu umuhimu wa kudumisha maadili mema na uhusiano mzuri kati ya jamii.
Amesema kuwa tabia ya kamari inaweza kuharibu uhusiano wa kifamilia na kusababisha migawanyiko katika jamii.