Gavana wa Marsabit Mohamud Ali apongeza rais Ruto kwa kuondoa hitaji la kupigwa msasa wakati wa kusaka kitambulisho….
February 6, 2025
NA JB NATELENG
Usajili wa watahiniwa wa kibinafsi ambao walikuwa wametarajiwa kuufanya mtihani wa kitaifa KCSE mwezi wa saba mwaka huu umeahirishwa.
Kulingana na mkurugenzi wa elimu kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kwamba usajili huu umeahirishwa baada ya kesi iliyowasilishwa mahakamani kuhusiana na mchakato wa kupinga watahiniwa wa kibinafsi kuufanya mtihani katikati ya mwaka wakisema kuwa haiafikiani na kanuni za baraza la mitihani nchini KNEC.
Magiri ambaye alizungumza na meza ya Radio Jangwani kwa njia ya simu ameelezea kuwa kwa sasa zoezi hilo la usajili litasitishwa hadi pale ambapo mahakama itatoa maamuzi kuhusiana na uhalali wa usajili huo.
Aidha Magiri amedokeza kuwa kufikia sasa wanafunzi wote jimboni Marsabit wameweza kufika shuleni na kuendelea na masomo huku akiipongeza juhudi ya serekali za kuhakikisha kuwa chakula kinapatikana katika shule zote jimboni.