Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na Isaac Waihenya,
Serekali ya kaunti ya kaunti inashughulikia swala la kuwepo kwa wataalam wa afya ya akili katika vituo vya afya mashinani.
Hili limefichuliwa na waziri wa jinsia katika kaunti ya Marsabit Jeremiah Ledanyi.
Akizungumza wakati wa zoezi la uzinduzi wa shirika la Open Minds Community Focus (OMCF)linashulikia maswala ya afya ya akili, waziri Ledanyi ametaja kwamba swala hilo limejadiliwa katika kikao cha mawaziri ili kuhakikisha kwamba serekali ya kaunti ya Marsabit inashughulikia kikamilifu maswala ya afya ya akili jimboni.
Aidha waziri Ledanyi amesema kuwa serekali ya kaunti itatenga fedha ili kuandaa vikao vya kutoa hamasa kwa wananchi kuhusiana na maradhi ya afya ya akili.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la Open Mind Focus Mariam Abduba ni kuwa shirika hilo litashughulikia haswa vijana na ambao kwa asilimia kubwa inakubwa na matatizo ya afya ya akili.
Amewataka vijana kufunguka na kusaka mswaada kwa wataalam husika kipindi wanapokumbwa na matatizo ya afya ya akili.
Wakati wa zoezi hilo la uzinduzi,Mariam amewapogeza wote waliunga mkono wazo hilo linalolenga kubadilisha Maisha ya waliosahaulika hapa jimboni.