Rais Ruto asikitikia hali ya usalama nchini DRC haswa ukanda wa unaokaliwa na waasi wa M23.
January 27, 2025
NA GRACE GUMATO
Wito unazidi kutolewa kwa wakaazi ya Dukana na Balesaru kuishi kwa amani na kudumisha amani mipakani.
Akizungumza katika eneo la Dukana na Balesaru kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amewahakikishia wakaazi wa maeneo hayo kuwa oparesheni ya kuwaondoa wahalifu kutoka nchi jirani ya Ethiopia imeanza huku pia akiwasihi wakaazi wa eneo hilo kutowaficha au kuwakaribisha wahalifu hao manyumbani mwao….
Aidha kamishna huyo amesema kuwa serikali imepiga marufuku usafiri wa usiku katika eneo hilo hadi usalama utakapoimarishwa katika mipaka wa Kenya na Ethiopia
Wakati uo huo kamishna kamau amewataka wakaazi wa mpakani kutolipiza kisisa bali iipe muda serikali kukomesha uhalifu na mauaji hayo.
Anasema kuwa wahalifu wana mikakati ya kupiganisha jamii mbili kuu jimboni Marsabit kwa msingi wa kikabila suala analosema halifai kwani mhalifu hana kabila.
Hata hivyo Kamau amewahakishia usalama wakaazi wa eneo hilo na kuwataka kuwarudisha watoto shuleni akiahidi usalama utahimarishwa.
Ziara hiyo ya wakuu wa usalama katika kaunti ndogo ya Dukana inajiri wiki moja baada ya utovu wa usalama kushuhudiwa katika eneo hilo.
Watu wanane pia waliuawa kinyama na miili yao kuchomwa wiki mbili zilizopita katika eneo la Elle-dimtu walipokuwa wakisafiri kwa Lori.