Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na JB Nateleng & Naima Abdulahi,
Wakazi wa Marsabit wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya HPV kwani ndio chanzo kikuu cha ugonjwa wa saratani ya njia ya uzazi.
Haya ni kwa mujibu wa Mohamed Salat Gonjobe ambaye ni mtaalam wa masuala ya ugonjwa wa saratani katika hospitali ya rufa ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya Kipekee Salat amesema kuwa virusi vya HPV vinaweza vikasambazwa kupitia kufanya mapenzi na kumbusu mtu aliye na virusi hivyo huku akiwataka wananchi kubadili mtindo wa Maisha ambao huenda ukasababisha kuenea kwa virusi hivyo.
Salat amefafanua ya kwamba hapo awali ugonjwa huu haukuwepo jimboni Marsabit lakini kupitia kusafiri kwa watu katika sehemu mbali mbali nchini na kutangamana na watu tofauti, visa vya saratani ya njia ya uzazi vilianza kuripotiwa hapa jimboni.
Salat ameelezea kuwa swala la mapenzi ya jinsia moja(LQBTQ) pia linachangia katika kusambaa kwa virusi vya HPV.
Mtaalam huyu amesema kuwa virusi hivi vya HPV vinadhuru pia wanaume hivyo kutoa wito kwa wazazi, pamoja na serekali kuweza kuwapa chanjo wavulana pia ili kuwenza kuwakinga dhidi ya virusi vya HPV