Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na Caroline Waforo,
Onyo kali limetolewa kwa vijana wanaoendelea kuwahangaisha wakaazi mjini marsabit kwa kujihusisha na visa vya wizi.
Hii ni baada ya duka moja kuvunjwa usiku wa kuamkia leo katika eneo la 680 viungani vya mji wa Marsabit na mali ya dhamana isiojulikana kuibiwa.
Akithibitisha kisa hicho OCPD wa Marsabit ya kati Edward Ndirangu amesema kuwa wameandaa mkutano na chifu wa eneo hilo pamoja na wazee kutoka jamii ambao wametakiwa kusaidia katika kuwatambua vijana wanaohusika na visa hivi.
OCPD anasema kuwa watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kadhalika amewataka wakaazi kushirikiana na idara ya usalama kwa kutoa taarifa muhimu zitakazosaidia kukomesha visa hivyo.