Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na Isaac Waihenya,
Kuhubiri hakuhitaji Degree.
Ndio kauli ya Maimamu wa msikiti wa Jamia hapa mjini Marsabit Sheikh Mohamed Noor.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipee Sheikh Noor ameitaka serekali kutupilia mbali hitaji la viongozi wote wa kidini kuwa na cheti cha degree ili kuruhusiwa kuhubiri.
Sheikh Noor amelitaja hitaji hilo kama lisilofaa kwani swala la kuhubiri ni wito kutoka kwa Mungu na wala sio kusomea.
Amekariri kuwa hilo linalenga kuwaondoa viongozi wa kidini walioko kwa sasa na kisha kuwaleta wapya ambao hawatakuwa na uwezo wa kuikosoa serekali inapokwenda mrama.
Hata hivyo Sheikh Noor ameunga mkono swala la kupigwa msasa kwa viongozi wa kidini japo amelitaka kutotumika kuhujumu haki za kuabudu hapa nchini.