Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
NA ISAAC WAIHENYA
Jamii ya Marsabit imetakiwa kuwalinda wanyamapori pamoja na mazingira ili kuzuia mizozo kati ya wanadamu na wanayamapori.
Kwa mujibu wa mratibu wa maswala ya mazingira Justus Nyamu ni kuwa japo kaunti ya Marsabit haijaripoti visa vya uwindaji haramu ila bado ipo hoja ya kuhifadhi wanyama pori hao.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Nyamu amesema kuwa kwa sasa idadi ya ndovu katika kaunti za Isiolo, Samburu na Marsabit wamepungua hadi elfu 7.
Aidha Nyamu amelitaja swala la usalama kama jambo ambalo halihatarishi tu maisha ya wananchi mbali pia maisha ya wanyamapori.
Kwa upande wake msimamizi wa shirika la wanyama pori Kimei ameipongeza jamii kwa kulinda wanyama pori na kuwataka kuripoti visa vyovyote vya uvamizi wa wanyamapori vijijini.
Kimei amesema kwamba idara hiyo imeweka mikakati ili kuzui mizozo ya kati ya wanyamapori na wananchi.
Justus Nyamu maarufu Elephant man kwa sasa yupo hapa jimboni baada ya kusafiri kwa miguu kwa siku 50 hadi hapa jimboni Marsabit huku akitoa hamasa kwa jamii kuhusiana na utunzaji wa mazingira na wanyamapori haswa ndovu.