County Updates, Editorial, Local Bulletins, National News

JAMII YA MARSABIT IMETAKIWA KUTOWAFICHA WATOTO WANAOUGUA UGONJWA WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CEREBRAL PALSY NA BADALA YAKE KUWAPELEKA HOSPITALI WAPATA MSAADA.

Na Isaac Waihenya,

Jamii imetakiwa kutowaficha watoto wanaougua ugonjwa wa kupooza kwa ubongo maarufu Cerebral Palsy.

Kwa mujibu wa afisa wa afya ya jamii katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Zainabu Huqa ni kuwa jamii ya Marsabit bado inawaficha watoto wanaougua maradhi hayo huku akiwataka kuwapeleka katika vituo vya kiafya ili wapate msaada.

Akizungumza katika warsha ilifadhiliwa na shirika la Collaborative Center for Gender and Development (CCDG) na kuwaleta wahudumu wa afya wa nyajani (CHPs) pamoja na wahudumu wa afya wasaididi (CHAs) na maafisa wa kitengo cha afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Zainabu amesema kuwa kuwaficha watoto wanaougua ugonjwa wa kupooza kwa ubongo maarufu Cerebral Palsy ni kuhujumu haki yao.

Aidha Zainabu amewataka wananchi kuasi kuwaficha pia watu wanaougua maradhi ya afya ya akili huku akitaja kwamba hali hiyo inaweza tibika iwapo wanaougua watawasilishwa katika vituo vya afya mapema.

Amewataka wahudumu wa afya wa nyajani (CHPs) pamoja na wahudumu wa afya wasaididi (CHAs) ambao wamepata mafunzo kuwa mabalozi wema kwa kuhakikisha kwamba wanaeneza ujumbe mashinani na kuondoa dhana potovu ambayo huwataja watu wanaougua maradhi ya afya ya akili kama watu waliolaaniwa.

Subscribe to eNewsletter