Rais Ruto asikitikia hali ya usalama nchini DRC haswa ukanda wa unaokaliwa na waasi wa M23.
January 27, 2025
Na Isaac Waihenya,
Idara ya elimu katika kaunti ya Marsabit imeweka mikakati kabambe ili kuzuia visa vya uchomaji wa shule kutokea hapa jimboni.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa idara ya elimu imehakikisha kwamba iko makini ili kuzuia kutokea kwa visa vya shule kuchomwa kama inavyoshuhudiwa katika kaunti zingine hapa nchini.
Magiri alizungumza na idhaa hii baada ya kuandaa mkao na washikadau katika sekta ya elimu na idara ya usalama hii leo katika shule ya upili ya Moi Girls hapa jimboni Marsabit.
Aidha Magiri amefichua kuwa manaibu kamishana hapa jimboni wataandaa mikutano ya kiusalama na wakuu wa shule ili kuweka mikakati zaidi kuhusiana na usalama wa wanafunzi shuleni.
Kuhusiana na swala la mitihani ya kitaifa, mkuu huyo wa elimu jimboni amedhibitisha kwamba wamejiandaa kikamilifu.
Kuhusiana na swala la shule ya El-molo ambayo imeadhirika na maji, Magiri amesema kuwapia idara ya elimu imeweka mikakati kuhakikisha kwamba watahiniwa katika shule hizo pia wanakalia mitihani.