Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na Caroline Waforo,
Serikali ya kaunti ya Marsabit imekanusha madai ya ubaguzi katika utoaji wa ajira hivi maajuzi haswa kwa wahudumu wa afya.
Hii ni baada ya wauguzi wanagenzi kulalamika kuwa hakukuwa na uwazi katika utoaji wa ajira huku pia wakilalamika kutengwa.
Madai haya yamekanushwa na katibu wa serikali ya kaunti ya Marsabit Hussein Tari Sasura.
Na huku taarifa zikiibuka kuwa wafanyikazi wa vibarua hawajalipwa kwa kipindi kwa miezi 10 katika mwaka wa kifedha 2022-2023 serikali ya kaunti ya Marsabit sasa inasema kuwa ni swala ambalo linashughulikiwa.