County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

ARDHI ILIYONYAKULIWA NA MABWENYENYE HAPA JIMBONI MARSABIT INAFAA IREJESHWA MARA MOJA.-ASEMA MWANAHARAKATI WA KUPIGANIA HAKI ZA KIBINADAMU MOHAMMED HASSAN.

Na Caroline Waforo,

Serikali itawaachia ardhi baadhi ya watu wanaokalia kipande cha ardhi ya msitu wa Marsabit kama vile Hulahula na Karare.

Haya yamebainika leo wakati wa uzinduzi wa Kamati ya watumizi wa huduma za mahakama CUC kaunti ya Marsabit.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo hakimu mwanadamizi wa mahakama ya Marsabit Simon Arome amesema kuwa uamuzi huo uliafika baada ya mazungumzo ya kina kati ya washikadau husika.

Kwa upande msimamizi wa misitu jimboni Marsabit Kadiro Oche ni kuwa msitu wa Marsabit ulikuwa takribani ekari 19,000 lakini sasa umesalia ekari 15,000 kutokana na unyakuzi wa ardhi.

Naye mwanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu Mohammed Hassan ambaye pia ni mkrugenzi wa shirika la CCRD ameitaka ardhi iliyonyakuliwa na mabwenyenye kurejeshwa.

Maswala mengine yaliyoibuka kuhusiana na uchufuzi wa mazingira ni pamoja na matumizi wa karatasi za plastiki huku wadau wakiwataka watu wanaouza karatasi hizo kukamatwa  na wito wa wakaazi kuhamasishwa kuhusu marufuku ya utumizi wa karatasi hizo ukitakiwa kutolewa.

Subscribe to eNewsletter