Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na Talaso Huka,
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya usalama wa wagonjwa hii leo, wito umetolewa kwa serekali ya kaunti ya Marsabit kuingiliana kati na kutatua mgomo wa wahudumu wa afya unaoendelea kwa sasa ili kuhakikisaha kuwa wananchi wa Marsabit na haswa wanaougua wako salama.
Kilingana na mwanaharati wa kutetea haki za binadamu kaunti ya Marsabit Mohammed Hassan ni kuwa ni kinanya kuona kwamba ulimwengu unaadhimisha siku ya usalama wa wagonjwa ila katika kaunti ya Marsabit hali ya wagonjwa si salama kwani wahudumu wa afya wamesusia kazi.
Akizungumza na Radio Jangwani Mohamemed ameilaumu serekali ya kaunti kwa kile amekitaja kuwa kutojali wananchi wake.
Aidha Mohamed ameitaka serikali ya kaunti ya Marsabit kutimiza matakwa ya wahudumu wa afya ili waweze kurejea kazini kuwahudumia wananchi.
Vilevile amehimiza jamii ya Marsabit kusaka matibabu kipindi wanapougua badala ya kupuuza na kisha kujuta baadae.
Kuhusiana na ugonjwa wa kupooza kwa ubongo maarufu Cerebral Palsy mwanarakati huyo wa kutetea haki za binadamu hapa jimboni Marsabit ameitaka jamaa kutowaficha watoto wanaougua maradhi hayo na badala yake kuwapekeleka katika vituo vya afya ili wapate kusaidika.