WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Isaac Waihenya
Idara ya usalama katika kaunti ya Marsabit itaaza zoezi la kuwapiga msasa watakaopewa nafasi za maafisa wa akiba yaani NPR mwishoni mwa mwezi huu wa Januari.
Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa kaimu kamishna wa kaunti ya Marsabit David Saruni ni kuwa zoezi hilo litafanyika kwa ushirikiano na wananchi ili kuhakikisha kwamba wataokabidhiwa majukumu hayo ni watu waaminifu na watakao yatekeleza kwa ubora wake.
Kuhusiana na Video inayosambaa mitandaoni inayoonyesha wezi wa mifugo wakiwaiba mifugo usiku wa manane,Saruni ametaja kuwa uchunguzi tayari umeanzishwa ili kuwatia baroni wahalifu hao.
Aidha mkuu huyo wa usalama jimboni alitoa wito kwa wananchi kusitisha swala la wizi wa mifugo huku akiwaonya watakaopatikana wakiendeleza uhalifu huo.