County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Wanafunzi wote waliofanya mitihani ya kitaifa ya Gredi ya 6 na KCPE mwaka jana katika kaunti ya Marsabit lazima waendelee na elimu.

Picha; Hisani

Na Isaac Waihenya,

Serekali itahakikisha kwamba wanafunzi wote waliofanya mitihani ya kitaifa ya Gredi ya 6 na KCPE mwaka jana wanaendelea na elimu yao.

Kwa mujibu wa kaimu kaunti kamishina wa Marsabit George Kamweru ni kuwa ni haki ya kila mwanafunzi aliyefanya mtihani wa gerdi ya sita kujiunga na Junior Secondary sawa na waliokalia mtihani wa KCPE kujiunga na kidato cha kwanza.

Akizungumza Ofisini mwake hii leo Kamweru ametaja kwamba serekali kupitia machifu itahakikisha kwamba wanafunzi wote wanaendeleza masomo yao huku akiwaonya watakaokaidi agizo hilo kwa kuendeleza mila potovu kama vile ukeketaji na ndoa za mapema.

Kamweru amewahakikishia wazazi pamoja na wanafunzi usalama wao haswa wakti huu shule zinapofunguliwa kwa muhula wa kwanza mwaka wa 2023.

Aidha mkuu huyo wa usalama jimboni amesema kwamba serekali itahakikisha kuwa wanafunzi wanapata chakula ili kuwawezesha kuendelea na elimu yao bila kutatizika.

Subscribe to eNewsletter