County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Viongozi wa jamii ya Rendille wakashifu vikali mauaji yaliyofanyika eneo la Yell Kurkum eneo bunge la Laisamis.

Aliyekuwa mgombea wa kiti cha Ugavana katika kaunti ya Marsabit, Sunya Orre ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa jamii ya Rendille.
Picha; Hisani

Na Emmanuel Amalo,

Viongozi wa jamii ya Rendille wamekashifu vikali mauaji yaliyofanyika eneo la Yell Kurkum eneo bunge la laisamis.

Wakizumgumza na vyombo vya habari  jijini la Nairobi  wakiongozwa na aliyekuwa anawania kiti cha Ugavana Sunya Orre viongozi hao waliitaka serikali  kuchukua hatua kali kwa wahusika.

Aidha wanaitaka serikali  kurejesha polisi ya Akiba NPR na pia kuweka kituo cha polisi kwenye eneo inayoshukiwa kutokea mashambulizi ili kukabiliana na majambazi.

Haya yanajiri baada ya Watu wanane kuuwawa kwenye uvamizi wa wizi wa mifugo uliofanyika alhamisi alfajiri wiki iliyopita na idadi isiyojulikana ya ngamia kuibiwa.

Sunya Orre aliandamana na aliyekuwa mwaniaji wa kicha ubunge laisamis Elizabeth Pantoren, Stephen Lebarakwe,  aliyekuwa MCA wa Ngurnit Ali Barmnin na aliyekuwa mwanianiaji wa kiti cha useneta Alyce Kureiya.

Subscribe to eNewsletter