IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Isaac Waihenya,
Tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC imewaajiri walimu 56 katika kaunti ya Marsabit watakaohudumu katika shule 149 za umaa zitakazokuwa na shule za upili ngazi ya chini Junior Secondary.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa TSC tawi la Marsabit Sammy Loitakol ni kuwa walimu hao watasaidiana na wengine 131 walio kwenye mafunzo yaani Interns ambao wote wanafaa kuripoti shuleni tarehe mosi mwezi Februari mwaka huu.
Loitakol ametaaja kwamba walimu jimboni Marsabit wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha kwamba mfumo mpya wa elimi CBC unatekelezwa ipasavyo.
Akizungumza na Radio Jangwani Loitakol ametaja kuwa tume hiyo pia imewaajiri walimu 29 zaidi katika shule za msingi ili kutatua kero la uhaba wa walimu jimboni.
Aidha Loitakol amesema kuwa licha ya kwamba nyongeza hiyo haitafikisha kikomo swala la ukosefu wa walimu katika kaunti ya Marsabit ila itasaidia katika kutatua hilo na kuimarisha kiwango cha elimu jimboni.