VIONGOZI WA KIDINI MARSABIT WAMEITAKA JAMII KUZINGATIA MAADILI ILI KUEPUSHA VISA VYA MAUAJI VYA WANAWAKE NCHINI
November 5, 2024
Na Samuel Kosgei,
Ni afueni kubwa sasa kwa wakaazi wa Bubisa eneobunge la North Horr kaunti ya Marsabit baada ya mashine ya kusafisha maji kwa kutoa madini ya chumvi kuzinduliwa rasmi na shirika la PACIDA na washirika wake mjini humo.
Afisa mkuu mtendaji wa shirika la PACIDA Marsabit, Patrick Katelo amesema kuwa maji katika vibanda vya maji katika vijiji vya Bubisa sasa yako salama kwani kwa miaka mingi wananchi hapo wamekuwa wakiumia na magonjwa ya figo na saratani ya koo kutokana na sumu ya chumvi kwenye maji.
Amesema sasa visa vya saratani ya koo na matatizo ya figo vitapungua kwa kiasi kikubwa kwani utafiti awali ulionesha kuwa watu watatu wanaaga dunia kutokana na athari ya maji ya chumvi.
Msimamizi mkuu wa shirika la Cargo Human Care Fokko Doyen ambalo sasa litakuwa likisimamia mradi huo baada ya kupokezwa na Caritas Germany, amesema kuwa uzinduzi wa mashine hiyo ya kuondoa chumvi ni hatua kubwa kwani magonjwa ya saratani na figo sasa itakuwa historia.
Wakti huo uo Katelo ametaka jamii ya eneo hilo kulinda mradi huo kwani ni ya manufaa kubwa ikizingatiwa kuwa Zaidi ya familia 2000 itategemea maji hayo yaliyosafishwa.
Amebaisnisha kuwa Zaidi ya asilimia 90 ya maji ya visima kaunti ya Marsabit ina chembechembe ya chumvi ambayo kuulinga na shirika afya duniani WHO ni hatari kwa afya ya binadamu.
Wakaazi wa Bubisa wakiongozwa na chifu wao Joseph Jirma amesema kuwa hatua ya PACIDA kusaka wafadhili kutoka mataifa ya nje imewaletea afueni kwani kwa miaka mingi watu wengi waliumia kutokana na magojwa na akina mama kutembea muda mrefu kusaka maji ya kunywa.