KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Isaac Waihenya,
Onyo kali imetolewa kwa wanaopania kuvuruga usalama barabarani haswa katika barabara kuu ya Marsabit kuelekea Isiolo kuwa watakabiliwa kisheria.
Kaimu kaunti kamishina wa kaunti ya Marsabit George Kamweru ametoa tahadhari hiyo huku akitaja kwamba ni hatia kisheria kufunga barabara ya umaa au kuendeleza shughuli zote za kihuni au kigaidi barabarani humo.
Kauli yake mkuu huyo wa usalama katika kaunti ya Marsabit inajiri wakti wanafunzi wanarejea shuleni kwa muhula wa kwanza wa mwaka wa 2023.
Akizungumza na Idhaa hii Kamweru pia ametoa onyo kwa wezi wa mifugo jimboni kuwa chuma chao ki motoni na kwamba serekali itakabiliana nao vilivyo.
Kadhalika ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na asasi za serekali kwa kutoa taarifa kwao zitakazofanikisha vita dhidi ya kero la usalama hapa jimboni Marsabit.