County Updates, Local Bulletins

Mwanaume Anayetuhumiwa Kunajisi Mtoto Dukana Ashtakiwa Mahakama ya Marsabit

Mahakama ya Marsabit. PICHA | KWA HISANI

Na James Wanyonyi

Mwanaume mmoja wa umri wa makamao amefikishwa leo hii katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kumnajisi msichana wa umri wa miaka 16.

Badake Yattani alishtakiwa kuwa mnamo tarehe 21 mwezi wa Januari  mwaka huu pamoja na wenzake  ambao hawakuwa mahakamani wanadaiwa kutekeleza kosa hilo lokesheni ya Bulukh katika kaunti ndogo ya Dukana.

Akiwa mbele ya hakimu Simon Arome  mshukiwa alikana mashtaka  dhidi yake.

Mahakama imeagiza mtoto aliyenajisiwa kupelekwa katika kituo cha uokoaji kwa miezi mitatu kusubiri kuendelea kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikizwa tena Septemba 26 mwaka huu.

Wakati uo huo Dararo Wangana aliikishwa katika mahakama  iyo hiyo kwa kosa la ugemaji wa pombe haramu aina ya chang’aa.

Ameshtakiwa kwamba tarehe 25 mwezi Juni alipatikana na pombe hiyo haramu lita 30 huko Korr katika eneo bunge la Laisamis

Wangana alikubali shtaka hilo, mahakama vile vile ilimuachilia kwa thamana ya sh 10,000 pesa taslim.

Subscribe to eNewsletter